Serif
Sans serif
Monospace

bold|normal

-2|-1|N|+1|+2

Usanifishaji wa Kiswahili

Usuli

Usanifishaji wa lugha ya Kiswahili ulianza tangu mwaka 1930 ilipoundwa Kamati ya Lugha ya Afrika Mashariki. Suala la msingi ilikuwa ni kuteua lahaja mojawapo ya lahaja za Kiswahili zipatzo takriban kumi na tano.Kamati hii iliamua kuisanifu lahaja ya Unguja kama mojawapo ya lahaja za Kiswahili kwa kuzingatia kuwa lahaja ya Kiunguja ilikuwa imeenea katika sehemu kubwa ya maeneo ya bara hadi kufikia Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kandokando ya Ziwa Tanganyika maeneo ya Umanyema, Kivu, Katanga. Pia nchini Burundi hasa katika jiji la Bujumbura.

Kwa hiyo uundaji wa usanifishaji wa Kiswahili sanifu ulikabiliwa na matatizo mengi kutokana na lahaja zilizokuwapo na hivyo kufanya utekelezaji wake kusuasua na hivyo usiwe na mafanikio makubwa ya kuridhisha. Ulikuwapo upungufu mkubwa wa istilahi katika nyanja za elimu hasa kwa upande wa sayansi na teknolojia.

Msukumo mkubwa wa kuundwa kwa istilahi ulitokana na kuingizwa kwa maarifa mapya katika lugha ya Kiswahili kutoka katika lugha za kigeni. Uingizwaji huu ulihusisha lugha mbili yaani lugha chanzo (Kiingereza) na lugha lengwa (Kiswahili).

Mtindo huu unahusisha lugha zinazoendelea na lugha zilizoendelea za Ulaya. Njia iliyotumika ya kuunda istilahi ilikuwa ni ya kukusanya maneno kutoka katika lugha ya Kiingereza na kutafuta visawe vyake kwa lugha ya Kiswahili.

Kwa upande wa Tanzania baada ya kupata uhuru, chombo rasmi kilichopewa dhima ya kufanya kazi hii ya kukuza, kuratibu na kuendeleza lugha ya Kiswahili ni Baraza la Kiswahili la Taifa (Bakita) kwa mujibu wa Sheria ya kuunda Bakita ya mwaka 1967.

Baraza la Kiswahili la Taifa lilitumia kamati zake hasa kamati yake maalumu ya kusanifu lugha iliyojulikana kama Kamati ya Kusanifu Lugha (Kakulu). Kamati ya Kakulu ilijumuisha wajumbe kutoka Bara za Visiwani na walishirikiana katika kupata istilahi za masomo mbalimbali kwa ajili ya kuandika makala, majarida, vitabu na vipeperushi. Bakita lilichapisha orodha ya istilahi za Kiswahili zilizosanifiwa kama hatua ya awali ya kutayarisha kamusi za taaluma mbalimbali.

Baada ya Bakita kusanifu istilahi za taaluma mbalimbali wataalamu wa uyatarishaji wa Kamusi kutoka Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili (TUKI) Chuo Kikuu cha Dar es Salaam waliendeleza kazi ya kusanifu lugha ya Kiswahili kwa kutayarisha kamusi za kitaaluma na hatimaye kuchapisha kamusi mbalimbali kama Fizikia, Kemia, Biolojia, Lugha na Isimu, Historia, Tiba, Sheria, Biashara na Uchumi. Kamusi hizi bado ni ndogo na ambazo kama zikiboreshwa na kuongezewa istilahi nyingi za kutosha, itakuwa ni hazina kubwa katika medani ya usanifishaji wa Kiswahili hasa kwa waandishi na wachapishaji vitabu vya taaluma.

Kama ilivyoelezwa hapo awali, kulikuwa na kazi ya kuunda istilahi za Kiswahili iliyoanzishwa mwaka 1930 na ilishika kasi nchini Tanzania baada ya serikali kuamua kuwa Kiswahili ni lugha rasmi na pia ni lugha ya taifa. Vilevile Kiswahili kilitangazwa kuwa ni lugha ya kufundishia katika shule za msingi na pia ni somo la lazima katika shule za sekondari na vyuo vya ualimu.

Katika kukabiliana na hali hii, Baraza la Kiswahili la Taifa (Bakita) lilianzishwa kwa Sheria ya Bunge jukumu la kusimamia, kuratibu na kukuza lugha ya Kiswahili katika ofisi za serikali na mashirika ya umma. Mashirika kama Taasisi ya Elimu, Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili, Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima na Idara ya Kiswahili Chuo Kikuu yaliundwa na yalishirikiana na Bakita katika kuunda istilahi.

Katika kutekeleza azma ya kukidhi mahitaji ya Kiswahili katika elimu, uendeshaji wa shughuli za serikali na mashirika ya umma ilikuwa ni lazima kuorodhesha maneno ya Kiingereza na kupata visawe vyake kwa lugha ya Kiswahili. Orodha ya maneno ya mapya yalisaidia katika kuandika vitabu vya kufundishia na kujifunzia. Njia zilizotumika kupata visawe ni hizi zifuatazo:

Kupata maneno kutoka katika Kiswahili chenyewe, kwa mfano:

Maneno yaliundwa kwa njia hii ni mengi sana.

Lahaja za Kiswahili nazo zimechangia kwa kiasi fulani kwa baadhi ya istilahi ijapokuwa utafiti wa kina haujafanyika. Mifano kutoka katika lahaja za Kiswahili kama Kiamu, Kipemba ni kama vile:

Hapa inabidi kujikita sana katika lahaja za Kiswahili kama vyanzo vya istilahi za Kiswahili.

Hatua nyingine ni katika kupata istilahi kutoka katika lugha za Kibantu. Hii ni kazi pevu inayohitaji utafiti wa kina na ambao bado haujashika kasi. Bakita limeweza kupata maneno machache kutoka katika lugha za makabila mbalimbali ya Tanzania kama Wanyakyusa, Wagogo, Wachagga, Wahaya, Wasukuma, n.k. Hata hivyo yafaa utafiti uendelezwe katika lugha nyingine za Afrika Mashariki ili lugha hii ionekane kama ni ya wananchi wa Afrika Mashariki.

Kwa mfano:

Kutoka katika lugha za makabila mengine ambayo si ya Kibantu imewezekana kupata maneno machache kutoka kwa kabila la Wamasai. Maneno mengi kutoka kwa kabila hili yametokana na uzoefu walio nao kama wafugaji. Kwa hiyo yako maneno ambayo ni visawe vya maneno ya kitaalamu hasa kwa upande wa Biolojia. Kwa mfano:

Inawezekana ziko njia ya finyanzo ambazo ni ngeni kwa watu wengi lakini Bakita wameona wafuate mfumo wa kuunganisha viambishi vya maneno ili kuunda istilahi. Kwa mfano:

Hatua nyingine ambayo haipendelewi sana na baadhi ya mashabiki wa lugha ya Kiswahili ni uundaji wa maneno mapya kutoka katika lugha za kigeni na kuyafanya yaandikwe na yatamkwe kwa kutumia misingi ya Kiswahili. Tunasema ni hatua ya kutohoa (utohozi). Maneno haya yanaandikwa kwa kuzingatia misingi ya lugha ya Kiswahili ni kama haya yafuatayo:

Mifano iko mingi na kwa wale wanaotaka kufuatilia zaidi wanaweza kupata kitabu cha Kiswahili cha Istilahi za Kiswahili kilichochapishwa na Bakita mwaka 2005.

Hebu tuangalie ijapokuwa kwa muhtasari suala la ukuzaji wa istilahi za Kiswahili kwa upande wa Kenya. Nchini Kenya usanifishaji ni suala tata kama alivyowahi kuandika Polome mwaka 1967 na kusema,

"Nchini Kenya kuna makabila ambayo yanajali zaidi lugha yao ya asili na utamaduni wao kuliko Kiswahili."

Profesa Wangari Maathai aliwahi kusema,

"Kiswahli hakijawahi kukubalika miongoni mwa Wakenya wengi. Wanatakiwa kuacha hisia za ukabila na kama Kiswahili hakitatiliwa mkazo na kuwa ni fahari ya Wakenya, ukuzaji wake utasuasua. Kwa bahati mbaya Kiingereza kina hadhi kubwa zaidi ijapokuwa Kiswahili ni lugha rasmi na pia ni lugha ya taifa".

Inafahamika kuwa kukua kwa utalii nchini Kenya kumedhoofisha ukuaji wa Kiswahili kwani mkazo unatiliwa katika matumizi ya Kiingereza na kuliko Kiswahili. Yafaa ikubalike kuwa Kiswahili ni lugha inayoweza kuwaunganisha wananchi wa Kenya na kuwafanya wamoja.

Kubwa zaidi ni kutokuwapo na chombo cha kitaifa cha kusimamia na kuratibu Kiswahili. Uanzishwaji wa chombo kimoja cha kuratibu Kiswahili kama Tume ya Kiswahili la Afrika Mashariki kutakuwa na mafanikio kama chombo cha kitaifa kitaundwa ili kufuatilia, kuhimiza na kukuza maendeleo ya Kiswahili nchini Kenya. Ni jambo la kufurahisha kuona kuwa lugha ya Kiswahili inatiliwa mkazo sasa hasa baada ya katiba ya Kenya kutamka kuwa Kiswahili ni lugha ya taifa na haina budi kutiliwa mkazo katika maisha yote ya Wakenya.

Kwa upande wa Uganda, lugha ya Kiswahili imebaki kutumika zaidi katika Jeshi la Uganda na pia Polisi. Kwa kiwango cha kitaaluma somo la Kiswahili linafundishwa katika baadhi ya vyuo vikuu hasa Chuo Kikuu cha Makerere.

Nchi nyingine kama Rwanda na Burundi bado zinasuasua na hazina sera madhubuti za lugha.

stephenjmmaina1965@yahoo.com

Источник: http://www.mwananchi.co.tz/